Mwanamziki mmoja aliyejibadilisha jinsia kutoka mwanume hadi mwanamke huko nchini Ukraine amezuiliwa kutoka katika taifa hilo na kuambiwa abaki apiganie nchi yake baada ya serikali ya Ukraine kuamrisha wanaume wote kutohama taifa hilo kwa sasa ili kusaidia wanajeshi wa nchi hiyo kupambana na vikosi vya Urusi.
Kupitia mtandao wake wa Instagram Jamaa huyo anayetambulika kwa jina la Zii Famelu mwenye umri wa miaka 31 kwa mda sasa amekua akiilalamikia serikali ya Ukraine kumruhusu aondoke nchini humo kwani yeye sasa ni mwanamke.
Zii Famelo amesema kwamba amezuiliwa asitoke nchini humo maana passport yake inamuonyesha kwamba yeye bado ni mwanaume.