Home dunia Amshtaki Mwanamume Kwa Kutofika Kwa “Date”

Amshtaki Mwanamume Kwa Kutofika Kwa “Date”

193
0

Mwanamke mmoja kutoka jimbo la Michigan nchini Marekani amemfungulia mashtaka mwanamume mmoja akitaka kulipwa dola elfu 10 za Marekani, ambazo ni sawa na shilingi milioni 1.1 pesa za Kenya, baada ya mwanamume huyo kutofika kwa “date” waliyokua wamepanga.

Mwanamke huyo kwa jina Qashontae Short amemshtaki Richard Jordan kwa madai ya kumuumiza kihisia na kumsababishia msongo wa mawazo, baada ya kutofika katika hoteli waliyokua wamekubaliana kukutana kwa ajili ya kupalilia hisia zao za mapenzi.

Kulingana na stakabadhi za mahakamani kuhusu kesi hiyo, Bi. Qashontae anadai Richard alimuumiza hisia kimaksudi kwa kutoka fika katika makutano yao.

Previous articleKing Saha Ajinunulia Zawadi Ya Bei Ghali.
Next articleBurna Boy: ‘Last Last’ Wimbo Bora Wa Safari Yangu Ya Mziki
Teddy Mwanamgambo is a media personality in the coast region. He has worked in different media houses over a period of time.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here