Jamaa mmoja raia wa Ujerumani ameingia katika vitabu vya rekodi duniani baada ya kufanikiwa kuvunja nazi 148 kwa kutumia mkono wake mmoja, katika mda wa dakika moja.
Muhamed Kahrimanovic, ameweka rekodi hiyo mpya katika kipindi kilichokua kikipeperuushwa moja kwa moja katika kituo kimoja cha runinga nchini Italia.
Katika jaribio hilo la kuweka rekodi, Kahrimanovic alifanikiwa kuvunja nazi moja katika kila pigo la mkono wake.