Home dunia Amchinja Mkewe Sababu Ya “Huruma”. Mahakama Yamwachilia Huru.

Amchinja Mkewe Sababu Ya “Huruma”. Mahakama Yamwachilia Huru.

153
0

 

Jamaa mmoja aliyemchinja mkewe na kumuua kabla ya jaribio lake la kujitoa uhai kutibuka ameachiliwa na mahakama moja nchini Uingereza, baada ya kutopatikana na hatia ya kuua kimaksudi.

Graham Mansfield, kutoka mji wa Manchester nchini Uingereza ameeleza mahakama jinsi alivyomchinja mkewe kwa jina Dyanne aliyekua na umri wa miaka 71 sababu ya mapenzi makubwa kwake, baada ya kumuona akiteseka akiugua ugonjwa wa saratani.

Mansfield amejitetea kuwa mkewe ndiye aliyemuomba amtoe uhai ili apumzike mateso na maumivu ya kuugua saratani isiyo na tiba na alimuahidi pia yeye atajiua ili waendeleze ndoa kuzimu; lakini jaribio lake la kujitoa uhai halikufanikiwa.

Mahakama imeamua kwamba Mansfield hakuua kimaksudi bali alilazimishwa kutekeleza mauaji na kumpatia “kifungo-hewa” cha miaka miwili, ambacho atakitumikia iwapo tu atafanya kosa lengine lakini kwa sasa yupo huru.

Previous articleMama Atishia Kumdhuru Mpenzi Wa Mwanawe Anayetumiwa Elfu 56 Kila Mwezi Na Mwanawe Iwapo Anamchezea Kihisia.
Next articleMahakama Yataka Kunyongwa Kwa Mfungwa Kupeperushwe “Live” Katika Runinga.
Teddy Mwanamgambo is a media personality in the coast region. He has worked in different media houses over a period of time.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here