Sasa ni rasmi kwamba Jennifer Lopez na Ben Affleck walifuna ndoa ya kisiri baada ya cheti chao cha ndoa kupatikana na kusambazwa mitandaoni.
Kulingana na ushahidi wa cheti hicho, Jennifer Lopez na Ben Affleck walifunga ndoa Jumapili ya tarehe 16 mwezi uliopita wa Julai katika kanisa moja dogo jimbo la Las Vegas usiku.
Ndoa yao ilifungwa na padri kwa jina Ryan Wolfe huku shahidi wao akiwa jamaa kwa jina Kenosha Booth na Jennifer alikubali kuadili jina lake hadi Jennifer Affleck.