Mwanamke mmoja raia wa Austria amezua gumzo barani Uropa baada ya kuripotiwa kwamba alisafiri na ing’e 18 bila kujua kutoka taifa la Croatia alikokua amekwenda kwa mapumziko.
Kituo kimoja cha kuhifadhi wanyama wa mwituni kwa jina Tierhilfe Gusental nchini Austria kimefichua kuwa mwanamke huyo alisafiri na ing’e hao katika begi lake la nguo na aligundua uwepo wa ing’e hao baada ya kufika nyumbani kwake.
Kituo hicho kimeeleza kuwa ing’e hao sasa wataachiliwa katika misitu ya taifa hilo badala ya kurudushwa nchini Croatia walikotokea.