Ne-Yo Ataka Kutosumbuliwa Na Mashabiki Akipambana Na Kashfa Ya Kuchepuka.
Msanii Ne-Yo kutoka nchini Marekani sasa anawataka mashabiki kuwacha kumfuatilia na maswali na kumpa nafasi ya kushughulikia kashfa ya kuchepuka inayomwandama faragani na mkewe.
Mke wa Ne-Yo kwa jina Crystal Renay mwenye umri wa miaka 42 amemweka Ne-Yo katika kashfa nzito baada ya kufichua kuwa Ne-Yo amewahi kuchepuka mara kadhaa katika miaka yao minane ya ndoa.
Ne-Yo sasa amewaomba mashabiki kumpa nafasi yeye na mkewe kushughulikia tofauti zao faragani kwani maswala kama hayo hayawezi kushughulikiwa katika majukwaa ya umma.