Msanii Nay wa Mitego kutoka Tz ametoa wito kwa washikadau wa sanaa nchini Tz kuchanga na kumnunulia gari mrembo Wema Sepetu.
Nay wa Mitego anasema Wema Sepetu ni mmoja kati ya warembo maarufu nchini Tz ambao wamechochea vyema ndoto za warembo wengi wa kizazi cha sasa kwenye Sanaa nchini humo na anafaa kutambuliwa na kuenziwa mbali na kuheshimiwa.
Kauli ya Nay Wa Mitego inajiri baada ya mrembo Wema Sepetu kulia mitandaoni baada ya kukejeliwa na baadhi ya washikadau wa burudani nchini humo, ilipobainika hadi sasa hamiliki gari lolote licha ya umaarufu wake.