Home BURUDANI “Rambo” Aombwa Talaka Na Mkewe Wa Miaka 25

“Rambo” Aombwa Talaka Na Mkewe Wa Miaka 25

146
0

Mke wa muigizaji maarufu wa filamu duniani Sylvester Stallone aka Rambo kwa jina Jennifer Flavin ameomba kupewa talaka ili kutamatisha ndoa yao iliyodumu miaka 25.

Bi. Flavin amefika mahakamani akidai talaka huku kiini cha kukosana kwao kikiwa bado hakijabainishwa.

Tetetsi za mkwaruzano wao zilichipuka baada ya Rambo kufuta tattoo ya sura ya Bi. Flavin aliyokua amejichora mkononi na kubadilisha na ya mbwa wao wanayefuga pamoja.

Kwa sasa Bi Flavin aidha anataka Rambo kuzuiliwa na mahakama kuficha baadhi ya mali walizochuma wakiwa pamoja, ili zigawanywe kwa usawa talaka itakapopeanwa.

Previous articleDj Khaled Amuorodhesha “Allah” Miongoni Mwa Ma’ Producer Wakuu Wa Album Yake Mpya.
Next articleCucumber Ndefu Zaidi Kuwahi Kuvunwa Duniani.
Teddy Mwanamgambo is a media personality in the coast region. He has worked in different media houses over a period of time.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here