Mke wa muigizaji maarufu wa filamu duniani Sylvester Stallone aka Rambo kwa jina Jennifer Flavin ameomba kupewa talaka ili kutamatisha ndoa yao iliyodumu miaka 25.
Bi. Flavin amefika mahakamani akidai talaka huku kiini cha kukosana kwao kikiwa bado hakijabainishwa.
Tetetsi za mkwaruzano wao zilichipuka baada ya Rambo kufuta tattoo ya sura ya Bi. Flavin aliyokua amejichora mkononi na kubadilisha na ya mbwa wao wanayefuga pamoja.
Kwa sasa Bi Flavin aidha anataka Rambo kuzuiliwa na mahakama kuficha baadhi ya mali walizochuma wakiwa pamoja, ili zigawanywe kwa usawa talaka itakapopeanwa.