Home kwetu Mchungaji Apigwa Na Waumini Baada Ya Kuwashurutisha Kutoa Sadaka.

Mchungaji Apigwa Na Waumini Baada Ya Kuwashurutisha Kutoa Sadaka.

106
0

Mchungaji mmoja huko Embu anauguza majeraha mabaya baada ya kuambulia kipigo kutoka kwa waumini wake kisa aliwaamuru kila mmoja atoe sh 4,200 ili awafungulie Baraka za mwaka mpya.

Mchungaji huyo kwa jina James Mugo mwanzilishi wa kanisa la Wings of blessing African Church mjini Embu alikua akihubiri kwenye ibada ya kwanza ya mwaka wa 2022 ambapo aliwaamuru waumini watoe 4200 kila mmoja awafungulie Baraka za mwaka mpya la sivyo awalaani kwa kuwa wagumu kwa mwenyezi mungu.

Matamshi yake hayakupokelewa vizuri na waumini wake ambao waliungana kwa pamoja na kumpa kichapo kikali kilichomsababishia majeraha makali. Kwa sasa mchungaji huyo anaendelea kuuguza majeraha mabaya katika hospitali moja mjini Embu akiendelea kupata matibabu

Previous articleVita Vya Maneno Vya Zuka Baina Ya Mr. Seed Na Ringtone.
Next articleMarioo:Kauli Ya Shabiki Ndio Kipimo Halisi Kwa Msanii.
Teddy Mwanamgambo is a media personality in the coast region. He has worked in different media houses over a period of time.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here