Home dunia Wavutaji Wafika Mahakamani Wakidai Bangi Waliyouziwa Haina Stimu. Wanataka Kulipwa.

Wavutaji Wafika Mahakamani Wakidai Bangi Waliyouziwa Haina Stimu. Wanataka Kulipwa.

123
0

Kampuni moja inayojishughulisha na uuzaji bangi nchini Marekani imejipata kortini baada ya wateja wake wawili kuishtaki kwa kile wanachodai kama kuuziwa bangi isiyokua na “stimu.”

Jasper Centeno kutoka Long Beach na Blake Wilson kutoka Fresno wote wakaazi wa jimbo la California ambako uuzaji bangi umehalaishwa, wameishtaki kampuni kwa jina DreamFields Brands kwa kuwauzia bangi isiyowalewesha ama kuwashika vizuri.

Kupitia wakili wao, Jasper na Blake wanasema walidanganywa kupitia matangazo ya kibiashara ya kampuni husika kuhusu ukali wa bangi yake.

Wateja hao wanadai walikubali kutoa pesa nyingi kununua bangi ya bei ghali wakidhani inaviwango vya juu vya stimu lakini wamegundua haina ukali wowote kama inavyoelezwa katika mabango ya biashara.

Previous articleTajiri Akataa Kurithisha Familia Mali Yake. Utajiri Wake Aachia “Mungu”.
Next articlePapa Francis Asema Baadhi Ya Mapadri Na Watawa Huangalia “Porn.”
Teddy Mwanamgambo is a media personality in the coast region. He has worked in different media houses over a period of time.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here